No menu items!
More

    Mamboleo Mshairi X Leteipa the King – Kumekucha Lyrics

    Mamboleo Mshairi X Leteipa the King – Kumekucha Lyrics
    #INTRO
    Iyeiyeeaaah
    Uwouwouwooooh
    Lalalalalalalalalalaaaaaa

    #CHORUS
    Kumekucha waambie
    Waskie
    Usisitize ili wayaskie
    Wasichana wa Afrika
    Tujivunie
    Ukeketaji nao tuutupilie
    Kumekucha waambie
    Waskie
    Usisitize ili wayaskie
    Wasichana wa Afrika
    Tujivunie
    Ukeketaji nao tuutupilie

    Kumekucha
    Tuwafwate ili kuwaokoa
    Na kuwakomboa
    Kama una mawazo ya zamani
    Sasa toa,
    Kumekucha
    Jifunue blanketi ulilojifunika
    Blanketi lililokutia kwenye giza
    La kuwakeketa
    Giza lililowanyima Raha
    Na urembo wao wa kumeremeta
    Kumekucha
    Amka kabla jamii yetu
    Itiwe makucha
    Tunajua hii ni Mila ya zamani
    Ila sasa Haina dhamani
    Zamani ilikuwa kwao ni hatari
    Lakini sasa kwa wasichana wetu
    Ni hatari
    Na wanasema
    Zoa mchele kabla ndege
    Hawajadona
    Hebu ona,
    Ona maelfu wanavyoangamia
    Kwa kumwaga damu
    Ona magonjwa yanavyozagaa
    Kwa ukeketaji
    Kama bado hujaona
    Hutaona
    Ila waambie,
    Kumekucha

    #CHORUS
    Kumekucha waambie
    Waskie
    Usisitize ili wayaskie
    Wasichana wa Afrika
    Tujivunie
    Ukeketaji nao tuutupilie
    Kumekucha waambie
    Waskie
    Usisitize ili wayaskie
    Wasichana wa Afrika
    Tujivunie
    Ukeketaji nao tuutupilie

    #CHORUS
    Mnavyozidi kuwakeketa
    Ndivyo jamii yetu inazidi kuchomeka
    Tunavyozidi kuwalazimisha wao kuoleka
    Kwa wazee waliozeeka
    Ndivyo jamii yetu inazidi
    Kubomoka tulikoezeka
    Simama Leo
    Kuwa mwangaza unaoangaza
    Kwani,
    Taa huwashwa ili kuwekwa peupe
    Kumekucha
    Tazama uzazi unavyokuwa kazi
    Tazama magonjwa kama Fistula
    Yanavyotisha kuwala
    Kumekucha
    Machozi yao kwangu
    Nikama kwaruzo la pini
    kwenye ini
    Damu yao itaturudia
    Kama mizimu ndotoni mwetu
    Uwepo wao utatoka
    Vijijini mwetu
    Najua jamii zetu
    Na tamaduni zetu
    Ni tamu kama asali
    Lakini kunazo ambazo Zina uchungu
    Wa pilipili
    Kumekucha

    #BRIDGE
    Leo ni Leo
    (Kumekucha )
    Leo ni Leo
    (Kumekucha )
    Leo ni Leo ooooh
    (Kumekucha )
    (Kumekucha )
    Leo ni Leo
    (Kumekucha )
    Leo ni Leo
    (Kumekucha )
    Leo ni Leo
    (Kumekucha )

    #VERSE
    Tuungane nchi na nchi
    Gambia Hadi Zambia
    Tanzania wenye nia
    Libya walete sura mpya
    Nigeria na Algeria
    Maanake
    Pamoja tunaweza kumaliza ukeketaji
    Wa mtoto wa kike
    Leo ni Leo
    Kumekucha

    Advertisement

    Lucas Roque e Gabriel...

    Homem de Branco - Lucas Roque e Gabriel Letra,...

    La China – Corazón...

    La China - Corazón de Cartón ( Letra )...

    LLEFLIGHT – FREESTYLE 2...

    LLEFLIGHT - FREESTYLE 2 ( Lyrics Broken) ( Lyrics...

    Lana Del Rey –...

    Lana Del Rey - Take Me Home, Country Roads...

    Luh Tyler – Change...

    Luh Tyler - Change My Wayz Letra...

    Larkin Poe – “Get...

    Larkin Poe - "Get Up" from the "Sweetwater" Soundtrack...

    Leteipa the King X Greg X Becca – Change the world

    Leteipa the King X Greg X Becca - Change the world Lyrics #VERSE When you see the world With open eyes When you see the time and how it...

    Bangi na supu – Leteipa the King Lyrics

    Bangi na supu - Leteipa the King Lyrics #INTRO Iyeiyeiyeeaaaaah Ni Vampk, 254 Traveller done #VERSE Najua uko busy na mambo zako Ila pokea simu, Hata dakika mbili tu Angalau Mwenzako nina...

    Lyrics Leteipa the King – Naila

    Lyrics Leteipa the King - Naila #INTRO Mhhhhhhh Ni Vampk 254 Big Daddy.. #VERSE Siku hizi namea kitambi, penzi tamu unalonipa. Kama kukupenda ni dhambi, mbinguni kamwe sitofika. Unanifanya niwe chongo, kipenzi weeh, Siku hizi wengine siwaoni. Unaponigusa...