Mbosso Ft Diamond Platnumz – Karibu

Mbosso Ft Diamond Platnumz – Karibu Lyrics Letra:
(Abbah), (Ayolizer)
Ishafika saba sasatunakungojea
Imebaki miezi miwili tu hebu siku sogea
Tuna shauku na bashasha ya kukupokea
Sio mimi na mama yako tu na bibi anakuombea

Mmmh! Imani yangu inanituma
Unanisikia baba yoo (Baba yooyoo)
Na furaha yangu dongo kumung’unya
Anapobugia mama yoo (mama yoo yoo)

Mmmm!, dalili wazi wazi
Kwa muda usha tawakal
Natamani useme zawadi
Ila acha ninunue vigari

Oooh kuna shangazi
Kibiti kwa mzee kikali
Ukiota meno ataleta viazi
Ule mihogo uwe ngangari
(Ule mihogo uwe ngangari)

Kwanza nitakupa jina gani
Talala talala lala talala
Kwanza karibu duniani baba
Talala talala lala talala

Kwetu furaha isiyo kifani
Talala talala lala talala
Ila kuna mengi duniani baba
Talala talala lala talala

Mmmh! kwa furaha niliyonayo
Ningechinja ng’ombe kwa tambiko
Ila baba yako uwezo sina
Pokea uji kwa kijiko
Pokea mwanangu (Ai yo yo)

Tena awape na habari
Waropokaji wapambe
We ni wangu wa halali
Wasije zani vya Nyange

Dunia ni mafuriko mvua kwote
Wanadamu mioyo ya matope
Ukitukanwa mwiko usiogope
Jikaze mwana wa Dangote

Ooh wasimuone
Kimasomaso wasimuone
Wenye jicho la chuki wasimuone mwanangu
Kimasomaso wasimuone

Ooh, wasimuone
Kimasomaso wasimuone
Wenye roho mbaya wasimuone
Kimasomaso wasimuone

Sa ringisha tumbo ringa, sa baby ringa
Waonyeshe ringa, wadolishie ringa
Sa ringisha tumbo ringa, oh baby ringa
Wao si wanazitoa, asa wadolishie ringa

Kwanza nitakupa jina gani
Talala talala lala talala
Kwanza karibu duniani baba
Talala talala lala talala

Kwetu furaha isiyo kifani
Talala talala lala talala
Ila kuna mengi duniani baba
Talala talala lala talala

Ndo namnyema mwanangu (Aiyoyo kwa baby shower)
Ooh rafiki kwa ndugu zangu (Aiyoyo kwa baby shower)
Furaha na uzazi wangu (Aiyoyo kwa baby shower)
Naringa ringa na mwanangu (Aiyoyo kwa baby shower)

Aiyoyo kwa baby shower
Aiyoyo kwa baby shower
Aiyoyo kwa baby shower
Aiyoyo kwa baby shower

%d blogueiros gostam disto: